fbpx

Pata mwanzo bora zaidi na mafunzo ya bure ya Kiingereza

Programu ya Kiingereza kwa Wahamiaji Watu Wazima

Jifunze Kiingereza cha kukusaidia kupata huduma, kufanya kazi, kusoma na kufurahia maisha yako ndani ya Australia.

  • Mpaka masaa 510 ya mafunzo ya bure ya Kiingereza
  • Jifunze Kiingereza kwa ajili ya kuishi, kufanya kazi na kusoma Australia
  • Fahamu kuhusu serikali na huduma za jamii
  • Masaa yasio na ukomo ya masomo ya bure ya Kiingereza
  • Pata marafiki wapya wakati unasoma
  • Pangilia mustakabali wako ndani ya Australia
  • Vigezo vya usajili vinatumika*

Tupigie leo kwa ajili ya taarifa za kuanza mafunzo yako ya BURE ya Kiingereza na STEPS kwa simu namba 1300 585 868

Kwa huduma za utafsiri, Pigia Huduma ya Utafsiri na Ufasili ya Taifa (Transalating and Interpreting Service au TIS) kwenye 131 450 kabla ya kupiga.

Muda wa madarasa unaoweza kubadilika kulingana na uhitaji

STEPS inatoa wa madarasa unaoweza kubadilika kulingana na mahitaji huko Casuarina and Palmerston – Tazama Ramani.

STEPS inakupa muda wa madarasa unaoweza kubadilika kulingana na mahitaji ili kukuwezesha kushughulika na mambo yako ya kifamilia, kazi au mambo mengine ya masomo. Una chaguo la kuhudhuria madarasa haya wakati wa mchana au usiku, katika siku na muda unaokufaa zaidi.

Madarasa ya Mchana: Jumanne, Jumatano, Alhamisi au Ijumaa, saa 2:45 asubuhi mpaka saa 9:15 alasiri
Madarasa ya Usiku: Jumanne, Jumatano au Alhamisi, saa 12 jioni mpaka saa 3 usiku

Programu ya Kiingereza kwa Wahamiaji Watu Wazima ni nini?

Programu ya Kiingereza kwa Wahamiaji Watu Wazima inafadhiliwa na Serikali ya Australia na hutoa masaa yasio na ukomo ya masomo ya bure ya lugha ya Kiingereza kwa wahamiaji wanaostahili na waingiaji kwa sababu za kibinadamu. Ikiwa umepewa viza ya kudumu au ya muda mfupi iliyo halali na unazungumza Kiingereza kidogo au huzungumzi kabisa, unaweza kustahili kwa ajili ya Programu ya Kiingereza kwa Wahamiaji Watu Wazima (Adult Migrant English Program au AMEP). Baadhi ya vijana wahamiaji wa umri kati ya miaka 15 na 17 wanaweza kukidhi vigezo vya kuipata pia. Fuatilia kuona ikiwa unakidhi vigezo vya kupata mafunzo ya BURE ya Kiingereza ndani ya Programu ya Kiingereza kwa Wahamiaji Watu Wazima.

Nitajifunza nini?

Kwenye AMEP utajifunza stadi za lugha ya Kiingereza ambazo zitakusaidia kukaa kwa mafanikio sana nchini Australia na watu wenye historia, malengo na uzoefu unaofanana. Utajifunza maadili ya Australia, utamaduni na sheria, na mambo mengi yatakayofanya iwe rahisi kwako kufanya kazi, kusoma na kufurahia maisha nchini Australia. Baadhi ya mada zinajumuisha;

  • mbinu za maisha, utamaduni, kupoteza familia au rafiki
  • afya na usalama
  • usimamizi wa fedha na benki
  • usafiri wa umma na udereva
  • mfumo wa utunzaji watoto na wa elimu
  • mfumo na huduma za matibabu
  • mifumo ya sheria
amep-logo

1300 585 868

Start typing and press Enter to search