Utunzaji Bure wa Watoto

Unahitaji huduma ya utunzaji mtoto ili uweze kuhudhuria mafunzo ya Programu ya Kiingereza kwa Wahamiaji Watu Wazima (Adult Migrant English Program au AMEP)? Huduma ya bure ya utunzaji watoto inapatikana kwa watoto walio chini ya umri wa shule wakati wa muda wako wa darasa.

Utakapokutana nasi tutajadili nawe chaguo la kufaa la kumtunza mtoto ili ufaidike zaidi na mafunzo yako.

Mafunzo ya Nyumbani

Wakufunzi wa nyumbani wanaweza kukupa msaada zaidi wa kujifunza nyumbani kwako. Usaidizi wa Mkufunzi Nyumbani ni BURE na unaweza kukupa usaidizi wa ana kwa ana unaohitajika kusaidia kuboresha ujuzi wako wa lugha. Tutakuunganisha na mkufunzi wa kukufaa kulingana na mahitaji yako ya kujifunza.

Mpango wa Lugha Makazi kwa Ajili ya Ajira na Mafunzo (Settlement Language Pathways to Employment and Training au SLPET)

Kukusaidia kuhamia kufanya kazi nchini Australia, unaweza kustahili kushiriki kwenye Mpango wa Lugha Makazi kwa Ajili ya Ajira na Mafunzo. Programu hii hukupa mpaka masaa 200 ya ziada ya mafunzo ya lugha ya Kiingereza yenye mkazo wa mafunzo ya Kiingereza kwa ajili ya ajira. SPLET hujumuisha pia mpaka masaa 80 ya uzoefu wa kazi ya muda kwenye tasnia mbalimbali, ili kukusaidia zaidi kuelewa mazingira na utamaduni wa mahali pa kazi wa Australia.

Programu Maalumu ya Maandalizi

Programu Maalumu ya Maandalizi hukupa mpaka masaa 400 ya ziada ya mafunzo maalumu ya Kiingereza kwa wateja wenye kustahili uhitaji wa kibinadamu kwa kutambua mahitaji yao makubwa zaidi ya usaidizi na mafunzo kutokana na hali yao ngumu ya uhamiaji, kama vile kupitia mateso au shida, na/au kuwa na elimu duni.

Madarasa kwa walio na umri chini ya miaka 18

Wahamiaji na walioingia kwa sababu za kibinadamu walio na miaka kati ya 15 na 17, ambao hawana ujuzi wa Kiingereza cha kufaa matumizi na ambao mahitaji yao hayafikiwi na mfumo wa kawaida wa shule, wanaweza pia kukidhi vigezo vya kushiriki kwenye programu. Ushiriki kwa ujumla huamuliwa kwa kila shauri peke yake, kwa kuzingatia hali ya mhusika mwenyewe na kwa kushauriana na shule za eneo husika.

Ikiwa unataka taarifa zaidi kuhusu huduma za ziada, tupigie kwenye namba 1300 585 868

Start typing and press Enter to search