Namna ya Kujisajili
- Tazama kuona kama unakidhi vigezo. Unaweza kutazama ukidhi wako wa vigezo mtandaoni au tupigie kwenye namba 1300 585 868.
- Jisajili nasi na weka ombi lako la kufanyiwa tathmini ya lugha ya Kiingereza. Tunaweza kuzungumza darasa lipi litakufaa zaidi na usaidizi wowote unaoweza kuuhitaji. Wasiliana nasi kwaa namba 1300 585 868 au tembelea moja ya vituo vyetu.
- Anza mafunzo yako ya BURE ya Kiingereza.
Vitu vya kuleta wakati wa kukutana nasi
Tafadhali leta pasipoti yako na nyaraka za kusafiria.
Usaidizi wa utafsiri
Tutaandaa mtafsiri wa bure kwa simu ili kukusaidia wakati wa kikao chetu na tathmini ya lugha la Kiingereza. Ikiwa utachagua kumleta mtu unayemfahamu kufanya tafsiri ni sawa pia.