STEPS Elimu & Mafunzo hufunza lugha ya Kiingereza, kuandika na kusoma pamoja na stadi za hesabu kwa wanafunzi kutoka mataifa zaidi ya 50, kwenye maeneo kuanzia majiji, mikoani mpaka maeneo ya mashambani. Utofauti wa wanafunzi wetu na maeneo tofauti tunayoyahudumia yametufanya kuwa wabunifu wa mafunzo yaliyoundwa maalumu kuitikia mazingira tunayofanya kazi, na wabobezi kwenye utoaji mafunzo kukidhi mahitaji, mitindo na maadili ya kujifunzia kwa wanafunzi wetu.

Mkazo wetu wa ushirika kwenye tasnia na utoaji mafunzo usiojibana umefikia matokeo mazuri kwa wanafunzi wetu. Tunaamini kwamba kwa kushughulikia mahitaji ya wateja wetu tunaweza kuchangia kwa namna chanya mustakabali wa kijamii na kiuchumi wa jamii kwa ujumla.

STEPS Elimu & Mafunzo ni sehemu ya STEPS Group Australia Ltd., taasisi isiyo ya kibiashara ambayo imelenga na kukazia kuleta mabadiliko kwa kutoa fursa.

Pokea habari kutoka STEPS Elimu & Mafunzo

Start typing and press Enter to search