Mabadiliko katika Programu ya Kiingereza kwa Wahamiaji Watu Wazima

Mwezi Julai 2017, Serikali ya Australia ilibadili namna ambavyo wanafunzi wanaosoma kwenye Programu ya Kiingereza kwa Wahamiaji Watu Wazima wanatathminiwa. Wanafunzi waliokuwa wanatathminiwa chini ya mfumo wa Cheti cha Kiingereza cha Kuongea na Kuandika (Certificate of Spoken and Written English au CSWE) sasa watatathminiwa chini ya Mfumo wa Australia wa Kupima Ujuzi wa Msingi (Australian Core Skills Framework au ACSF).

Mfumo wa Australia wa Kupima Ujuzi wa Msingi (Australian Core Skills Framework au ACSF) ni nini

Mfumo wa Australia wa Kupima Ujuzi wa Msingi (Australian Core Skills Framework au ACSF), unapima kiwango chako cha ujuzi kwenye kujifunza, kusoma, kuandika, mawasiliano kwa mdomo na kuhesabu. Tunatumia njia hii pia kupima kiwango cha ujuzi wako wa lugha ya Kiingereza, na kutathmini uwezo wako wa kupata ajira na kufanikiwa katika kazi.

Manufaa ya Mfumo wa Australia wa Kupima Ujuzi wa Msingi

Mfumo wa Australia wa Kupima Ujuzi wa Msingi (Australian Core Skills Framework au ACSF) ni mfumo unaotambulika zaidi wa kupima ujuzi wa msingi kwenye elimu ya ustadi nchini Australia, na ndiyo utakaotumika zaidi kukupima wakati wa maombi ya masomo, mafunzo au ajira. Kubadili namna wanafunzi wa Programu ya Kiingereza kwa Wahamiaji Watu Wazima (Adult Migrant English Program au AMEP) wanavyotathminiwa kwenda Mfumo wa Australia wa Kupima Ujuzi wa Msingi (Australian Core Skills Framework au ACSF) kutaboresha uwezo wa wanafunzi kuwa na wigo mpana zaidi wa Mafunzo, elimu na fursa za ajira.

Mabadiliko haya yataniathiri vipi?

Wanafunzi wa Programu ya Kiingereza kwa Wahamiaji Watu Wazima (Adult Migrant English Program au AMEP) ambao walianza masomo yao kabla ya Julai 2017, na walikuwa wakitathminiwa chini ya mpango wa Cheti cha Kiingereza cha Kuongea na Kuandika (Certificate of Spoken and Written English au CSWE), sasa watatathminiwa kwa kutumia Mfumo wa Australia wa Kupima Ujuzi wa Msingi (Australian Core Skills Framework au ACSF). Masomo uliyohitimu kuelekea kupata Cheti cha Kiingereza cha Kuongea na Kuandika yatatambulika na mkazo wa masomo utabadilika kufuata Mfumo wa Australia wa Kupima Ujuzi wa Msingi.

Kwa wanafunzi walioanza masomo yao chini ya Programu ya Kiingereza kwa Wahamiaji Watu Wazima baada ya Julai 2017, moja kwa moja watatathminiwa chini ya Mfumo wa Australia wa Kupima Ujuzi wa Msingi (Australian Core Skills Framework au ACSF).

Maswali?

Kwa taarifa zaidi kuhusu mabadiliko haya unaweza kutuandikia barua pepe kwenda amep@stepsgroup.com.au au simu 1300 585 868. Kwa huduma za kutafsiri piga simu kwa Huduma ya Kutafsiri na Ukalimani (TIS National) kwenye namba 131 450 kabla ya kupiga simu.

Start typing and press Enter to search