Je, AMEP ni programu sahihi kwa ajili yangu?

AMEP inapatikana kwa wote waliokidhi vigezo vya viza ya kudumu wa umri wa miaka 18 au zaidi ambao hawana ujuzi mzuri wa lugha ya Kiingereza.

Upatikanaji wa programu umeongezwa kwa baadhi ya walio na viza ya muda mfupi kama ilivyobainishwa kwenye kanuni ya Kozi za Kiingereza kwa Walio na Baadhi ya Viza za Muda Mfupi. Madaraja ya viza za muda mfupi yanajumuisha:

 • Daraja F (WF)
 • Stadi za Biashara (ya mpito) (Daraja UR)
 • Stadi za Biashara (ya mpito) (Daraja EB)
 • Kutegemeana (ya mpito) (Daraja UG)
 • Mshirika (ya mpito) (Daraja UF)
 • Mshirika (ya muda mfupi) (Daraja UK)
 • Maazimio ya Hali (ya muda mfupi) (Daraja UH)
 • Mpango wa Mahali Salama (Daraja XE)
 • Mwenye Ujuzi–Eneo Tengefu–Aliyedhaminiwa (ya mpito) (Daraja UZ)
 • Mwenye Ujuzi-Huru Kieneo (ya mpito) (Daraja UX)
 • Mwenye Ujuzi-Kieneo Aliyedhaminiwa (daraja dogo 475)
 • Mwenye Ujuzi-Kieneo Aliyedhaminiwa (daraja dogo 487)
 • Mwenye Ujuzi-Kieneo Aliyedhaminiwa (daraja dogo 489)
 • Ya muda mfupi (Kuzingatia Ubinadamu) (Daraja UO); na
 • Ulinzi wa Muda Mfupi (Daraja XD)

Chini ya umri wa miaka 18

Wahamiaji na wanaoingia kwa sababu za kibinadamu wenye umri kati ya miaka 15 na 17, ambao hawana ujuzi mzuri wa Kiingereza na ambao mahitaji yao hayajafikiwa vizuri na elimu ya kawaida, wanaweza pia kukidhi vigezo vya kushiriki kwenye programu.

Ushiriki kwa ujumla huamuliwa kwa kila shauri, kwa kuzingatia hali ya mtu husika na kushauriana na shule za eneo husika.

Muda husika

Kushiriki kwenye proramu, wahusika wenye viza stahiki wanapaswa kukidhi matakwa ya muda kisheria kwa ajili ya usajili, uanzaji na umalizaji. Ukomo wa muda hapa chini unahusika kuanzia tarehe ya viza ya mnufaika mtarajiwa kuanza kutumika au tarehe aliyowasili nchini Australia, chochote ambacho ndicho kipya zaidi.

Miaka 18 na zaidi

 • Usajili ndani ya miezi sita.
 • Kuanza mafunzo ndani ya miezi 12.
 • Kuhitimu mafunzo ndani ya miaka mitano.

Chini ya miaka 18

 • Usajili na uanzaji mafunzo ndani ya miezi 12.
 • Kuhitimu mafunzo ndani ya miaka mitano

Kiingereza cha kufaa matumizi

Zaidi la ukomo wa muda kisheria, wenye viza stahiki wanapaswa pia kutathminiwa (na watu wenye utaalamu) kuwa wana ‘chini ya kiwango kinachofaa’ cha ujuzi wa Kiingereza kama ilivyoainishwa kwenye kitendea kazi kisheria cha ‘Utaratibu au Viwango vya Kiingereza cha Kufaa Matumizi’

Ikiwa una hakika unastahili mafunzo ya BURE ya Kiingereza, tupigie kwa namba 1300 585 868

Start typing and press Enter to search