fbpx

Namna ya Kujisajili

  1. Tazama kuona kama unakidhi vigezo. Unaweza kutazama ukidhi wako wa vigezo mtandaoni au tupigie kwenye namba 1300 585 868.
  2. Jisajili nasi na weka ombi lako la kufanyiwa tathmini ya lugha ya Kiingereza. Tunaweza kuzungumza darasa lipi litakufaa zaidi na usaidizi wowote unaoweza kuuhitaji. Wasiliana nasi kwaa namba 1300 585 868 au tembelea moja ya vituo vyetu.
  3. Anza mafunzo yako ya BURE ya Kiingereza.

Vitu vya kuleta wakati wa kukutana nasi

Tafadhali leta pasipoti yako na nyaraka za kusafiria.

Usaidizi wa utafsiri

Tutaandaa mtafsiri wa bure kwa simu ili kukusaidia wakati wa kikao chetu na tathmini ya lugha la Kiingereza. Ikiwa utachagua kumleta mtu unayemfahamu kufanya tafsiri ni sawa pia.

Kupata taarifa zaidi juu ya namna ya kujisajili tupigie kwa namba 1300 585 686 au tutembelee kwenye kituo cha karibu zaidi cha Programu ya Kiingereza kwa Wahamiaji Watu Wazima (Adult Migrant English Program au AMEP)

Kwa huduma za utafsiri pigia Huduma ya Utafsiri na Ufasiri ya Kitaifa (Translating and Interpreting Service au TIS) kwa namba131 450 kabla ya kutupigia

Start typing and press Enter to search